Wananchi wakiingia katika banda la Maliasili na Utalii katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba.
Mtaalamu wa Uenezi Katika Programu ya Panda miti Kibiashara(PFP), George Matiko akielimisha watu waliotembelea banda la PFP. hilo katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba.
Kushoto ni Afisa misitu Uenezi, Mahendeka Jeremiah (kulia) Afisa Misitu Uenezi Dorice Nkawamba Wakiwaelimisha washiriki wa maonesho ya sabasaba waliotembelea banda hilo kuhusu namna ya kujiunga na programu ya Panda Miti Kibiashara.
Katikati, ni kiongozi wa banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, Uzeeli Kiangi akiwa na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Gradness Mkamba (Kuhoto), na Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa Misitu na nyuki Monica Kyaga (kulia) walipotembelea banda la Panda la Miti Kibiashara.
Baadhi ya wananchi wakirudi kutoka katiaka sehemu ya wanyama pori hai ndani ya banda la Maliasili na Utalii. katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba.
Wananchi wakiwa ndani ya banda la Maliasili na Utalii.
Wananchi wa Nyanda za Juu Kusini wamefanikiwa kubadili kilimo cha miti kuwa cha kibiashara baaada ya kupata hamasa kupitia Programu ya PANDA MITI KIBIASHARA (Private Forestry Programme). Programu hiyo ambayo ilianzishwa mwaka jana (2014) na serikali za Tanzania na Finlandimewapatia wananchi mbegu bora za miti ya Misindano na Mikaratusi na elimu ya kuikuza miti hiyo katikavijiji 12 vya majaribio.
Hayo yalidhihirika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) katika Banda la PANDA MITI KIBIASHARA lililomo ndani ya Banda Kuu la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Alipokuwa anazungumza na watu waliotembelea banda hilo Mtaalam wa Uenezi wa Programu hiyo Bw George Matiko aliwashauri wananchikupanda miti kibiasharakama inavyofanyika sasa katika mikoa ya Njombe na Iringa na sehemu zingine za Nyanda za Juu Kusini.Alisisitiza ‘wakati sasa umefika wa kuthamini kilimo cha miti na kukuza miti kama zao la biashara’.
Katika msimu wa mvua wa mwaka huu (2015) miche iliyostawishwa na Programu hiyo ilipandwa na wananchi katika eneo la zaidi ya hekta 1,000. Kwa kuwa watu wengi wamehamasika, katika msimu ujao wakupanda miti, vijiji vingi zaidi vitashirikishwa kwenye Programu hiyo ambapo inategemewa kuwa zaidi hekta 2,000 zitapandwa miti.
Kwa kuanzia, Programu hii inafanya shughuli zake katika mikoa ya Njombe (wilaya za Njombe, Ludewa na Makete), Iringa (wilaya za Mufindi na Kilolo) na Morogoro (wilaya ya Kilombero).
Lengo kuu la Programu wa Panda Miti Kibiashara ni kuinua kipato cha wakulima wa miti kutokana na kupanda miti kibiashara. Programu ya Panda Miti Kibiashara inahimiza upandaji miti kwa kutumia mbegu bora na kutunza mashamba kitaalaamhadi miti ifikie umri wa kuvunwa.
Programu ya Panda Miti Kibishara inashirikiana na Vikundi vya Wakulima wa Miti (Tree Growers Associations – TGA) pamoja na watu wengine wanaopenda kupanda miti. Pia Programu hii inatoa misaada ya kupanda miti kwa watu binafsi na familia zao, wafanya biashara wadogo na wa kati, Taasisi za umma, vituo vya utafiti, taasisi za elimu, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) na Asasi za Jamii (CBO).
Vilevile, ili kuwawezesha wakulima wa miti kujiongezea kipato wakati wakisubiri miti waliyoipanda ifikie umri wa kuvunwa, Programu inawahimiza wakulima kufanya Shughuli za Kujiongezea Kipato (Income Generating Activities – IGA).
Kwa msimu wa mwaka 2015 hadi 2016 wakulima wa miti watapata misaada ya kutekeleza Shughuli za Kujiongezea Kipato zinazohusiana na Ufugaji Nyuki, Kilimo cha Viazi, Kilimo cha Parachichi (Avocado) na kilimo cha Maharage.–
Kwa msimu wa mwaka 2015 hadi 2016 wakulima wa miti watapata misaada ya kutekeleza Shughuli za Kujiongezea Kipato zinazohusiana na Ufugaji Nyuki, Kilimo cha Viazi, Kilimo cha Parachichi (Avocado) na kilimo cha Maharage.–
Post a Comment