Baada ya Uongozi wa Klabu ya Kimondo inayoshiriki ligi daraja la kwanza kudai mshambuliaji GEOFREY MWASHIUYA ni mali yao, Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliaji huyo baada ya kukamilisha usajili wake.
Kimondo kupitia kwa Mkurugenzi ERICK AMBAKISYE wameshangazwa na hatua ya Yanga kumtumia mshambuliaji huyo kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi yaSports Club Villa ya Uganda Jumamosi iliyopita wakidai kuwa bado ni mchezaji wao.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga JERRY MURO anasema MWASHIUYA ni mchezaji wao halali kwa sababu wamemsajili kwa kufuata taratibu zote.
Jerry Muro amesema ‘Geofrey amejitokeza hadharani amecheza mpira watu wakaanza kushtuka baada ya kuona dhababu imeanza kung’ara mimi nikashangaa, alikua anakaa hapa akaenda kuishi Tabata….. tumekaa nae muda huo wote, watu walikua wapi wasiseme ni mchezaji wao?’
‘Niwataarifu kanuni sheria na taratibu, mchezaji anapochezea ligi daraja la kwanza mchezaji mkataba wake unakwisha pale ligi inapokwisha, hata kama angekua na mkataba wale wa kule daraja la kwanza hawana mikataba ya miaka mitano au mitatu‘ – Jerry Muro
‘Tumekwenda TFF na kuuliza… hana mkataba na Kimondo, zile wanazosema ni fomu ambazo mchezaji anajaza ili acheze ligi daraja la kwanza apate kitambulisho kama zilivyo taratibu nyingine‘
Post a Comment