Klabu ya Manchester United ilifanikiwa kufanya usajili wa dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa na kumnyakua mshambuliaji mpya.
Mshambuliaji huyo ni Anthony Martial, mwenye miaka 21 na raia wa Ufaransa aliyekiwa katika klabu ya AS Monaco ya Ligue 1. Amesajiliwa kwa kiasi cha £36m.
United walikuwa wakitafuta mshambuliaji wa kumsaidia Wayne Rooney na kocha Louis Van Gaal aliahidi kusajili mshambuliaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Haikujulikana ni mshambuliaji gani hasa ingemsajili lakini bahati ikawa ya kinda huyo.
Van Gaal amesema haya kuhusu huyu mchezaji huyo:
Anthony ana kipaji cha asili, mdogo, foward mwenye uwezo wa aina tofauti uwanjani. Tulikuwa tunamuangalia kwa muda mrefu na ameendelea kuwa mchezaji mzuri ndani ya AS Monaco. Nina furaha amejiunga nasi nikiamini hii ni club bora kwake kuendelea kuwa mchezaji bora zaidi duniani. Anthony ana uwezo wa kuwa mchezaji bora kabisa kwenye ligi ya EPL japokuwa tunahitaji kumpa muda wa kuzoea mazingira ya ligi hii.
Post a Comment