Kushindwa kwake kwenye kura za maoni mkoani Singida hakumaanishi kuwa Wema Sepetu ameachana na masuala ya siasa.
Ikiwa ni siku chache tu baada ya kupokea matusi ya kila aina kwenye Instagram baada ya kuwaita wale wanaoiunga mkono Ukawa ‘hawajielewi, Miss Tanzania huyo wa zamani anaonekana kupewa mchongo na Rais anayeondoka madarakani, Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete akisalimiana na waigizaji Wema Sepetu na Steve Nyerere
Haijajulikana wazi ni kitu gani Wema na Kikwete kimewakutanisha leo kwenye ikulu ya mjini Dodoma, lakini huenda kikawa ni kitu kitakachompa mkwanja wa maana mrembo huyo.. walau kutokana na kile alichoandika.
“Wakati nyie mnaongea upuuzi… Yangu yaninyookea….. Alhamdulillah… Wa moja havai mbili… Abadan asilan…. Earlier today… Ikulu… Dodoma… Thank u Mr.President,” ameandika Wema kwenye picha akiwa na Kikwete.
Si Wema tu atakayenufaika na mishe za uchaguzi mwaka huu.
Wema amepost picha hiyo juu ya Steve Nyerere na kuandika:
Hongera sana ndugu yangu kwa kupewa nafasi hii kubwa… Nina imani hautotuangusha na yale tulioyapanga basi yatafanikiwa… Im so proud of you @stevenyerere2 … Haiya sasa twende tukatumikie jamii… Vijana wenzako tupo nyuma yako
Post a Comment