Diamond
Mashabiki wengi wa muziki wa Bongo wanatamani siku moja kuwaona Diamond na Alikiba wanafanya kazi pamoja, kama ambavyo Wizkid na Davido ambao wameahidi kuachia joint yao siku si nyingi baada ya kuthibitisha kuwa hakuna beef kati yao.
Upande wa Diamond amesema kuwa yupo tayari kufanya chochote katika muziki endapo kina maslahi kwake. Kuthibitisha hilo ametoa mfano kuwa alikubali kushiriki tamasha la ‘Kiboko Yao’ lililofanyika Leaders Club mapema mwaka huu ambalo na Alikiba pia alitumbuiza, kwasababu lilikuwa na maslahi mazuri kwake.
“Unajua mi nafanya biashara, na kitu chochote ambacho kwangu mi kinakuwa kina maslahi mi siwezi kukataa kukifanya.” Diamond ameaimbia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
Baba Tiffah ameongeza kuwa alilipwa shilingi milioni 100 ili kutumbuiza kwenye tamasha hilo.
“Nakupa mfano hapa katikati kulikuwa na show ilivyokuja mi nikawaambia hii show ni biashara kwangu mi sikatai lakini you have to pay me, show mi nimelipwa milioni 100 ndo nimetumbuiza, siamini kama kuna msanii wa kiTanzania alishawahi kulipwa milioni 100, hili swala si umetengeneza kama beef, tuifanye kibiashara, nikalipwa milioni 100, nisiwe mnafiki milioni 100 sababu show hizo natozaga nikiwa na show nje labda Kenya , Rwanda naweza nikapiga show milioni 120, 130 lakini ilikuwa mara ya kwanza Tanzania milioni 100, lakini kwasababu ilikuwa beef na sio kwamba show haikulipa, ililipa kwasababu ilikuwa imeshatengeneza tension yaani flani na flani kwahiyo tuzitumie hizi vitu kimaslahi zaidi.”

Post a Comment

 
Top