MSHAMBULIAJI aliyechemsha na kutemwa Simba, Danny Sserunkuma ameikacha timu yake ya zamani, Nairobi City Stars iliyotaka kumsajili na ameamua kutimkia katika moja ya klabu za Armenia.

Sserunkuma, mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) msimu uliopita akiwa na Gor Mahia, alihusishwa kujiunga na Nairobi City Stars katika usajili wa Juni mwaka huu, lakini ameshindwa kufikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo inayonolewa na Paul Nkata.

AFC Leopards pia ilihusishwa kutaka kumsajili mshambuliaji huyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Jumanne Juni 30.  
                                            
Mmoja ya mitandao ya michezo nchini Uganda, umeripoti leo kuwa Sserenkuma ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kutemwa na Simba Mei mwaka huu, yuko mbioni kujiunga na moja ya klabu za Ligi Kuu ya Armenian.

Mganda huyo alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Gor Mahia katika miaka miwili aliyokaa ndani ya klabu hiyo na kuwapa mataji mawili ya KPL 2013 na 2014.


Simba ilimtema mshambuliaji huyo kwa maelezo kwamba ameshindwa kuendana na mfumo wa uchezaji wa mabingwa hao mara 18 wa Tanzania Bara.

Post a Comment

 
Top