Msanii wa filamu Bongo, Steven Mengere, ‘Steve Nyerere'.
Chande Abdallah
MAKUBWA HAYA! Msanii wa filamu Bongo ambaye ameingia kwenye listi ya waliotangaza nia kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kinondoni, Steven Mengere, ‘Steve Nyerere’ amedaiwa kuajiri mlinzi wake binafsi ili kujihami na maadui wake wa kisiasa.
Steve alinaswa na paparazi wetu akiwa analindwa na ‘bodigadi’ kila alipokuwa akienda ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Dar kulikokuwa na hafla ya uchangiaji waandishi wa habari, Media Car Wash na aliweka wazi kuwa hiyo yote imetokana na uamuzi wake wa kuingia kwenye siasa.
“Nimeambiwa na wazee kuwa nisiwe peke yangu, si unajua tumeingia upande wa siasa, ni mambo ya kiusalama zaidi ndiyo maana nimemwajiri huyu,” alisema Steve Nyerere baada ya kuulizwa kuhusu suala hilo.

Post a Comment

 
Top