Mramba (kushoto) akiteta jambo na wakili wake, Peter Swai baada ya Mahakama kumhukumu miaka mitatu jela na faini ya shilingi milioni tano.
Harun sanchawa na denis mtima
JOTO ya jiwe! Wafungwa wawili wapya katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na mwenzake wa Nishati na Madini, Daniel Yona, wanadaiwa kukesha huku wakilia katika siku wakianza kutumikia kifungo chao cha miaka mitatu baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaa Jumatatu iliyopita.
Kutoka kushoto ni Basil Mramba,  Daniel Yona na Gray Mgonja wakiteta jambo.
Basil Mramba akionekana ndani ya defenda la Polisi kuelekea Gereza la Ukonga jijini Dar.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (katikati) akitoka katika chumba cha Mahabusu baada ya hukumu hiyo kutolewa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya gareza hilo, Mramba na Yona, ambao walikuwa mawaziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu tofauti, waliohukumiwa kifungo hicho na Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika katika kesi iliyochukua zaidi ya miaka nane tokea walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, wakiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati, Agrey Mgonja, muda mwingi walionekana watu wenye mawazo huku wakijifuta machozi machoni mwao.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa Basil Mramba na Daniel Yona wakiondoka katika Mahakama ya Kisutu kwa masikitiko makubwa baada ya kupelekwa gerezani.
“Nadhani hawakutegemea kama kweli watafika hapa, maana walionekana wenye huzuni sana. Lakini wakati wao wakiwa katika hali hiyo, wafungwa wengine walikuwa wakishangilia kwa sababu ni jambo geni kwao kuwaona  vigogo gerezani, hasa waliowahi kushika nyadhifa kubwa kama zao. Hali siyo nzuri kwa kweli,” kilisema chanzo hicho.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Gray Mgonja (katikati) akionekana mwenye furaha baada ya kuachiwa huru na Mahakama.
Katika kesi yao, mawaziri hao waandamizi walituhumiwa pamoja na mambo mengine, kutumia vibaya madaraka yao yaliyosababisha hasara ya shilingi bilioni 11 kwa serikali.
Lango kuu la Mahakama ya Kisutu kabla ya kuondoka defender la Polisi.
Hawa wanakuwa viongozi wa kwanza waliowahi kufikia ngazi ya uwaziri kuhukumiwa jela tokea kuondoka kwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye serikali yake ilimfunga aliyepata kuwa waziri Abdalah Fundikira (sasa aliyepata marehemu).

Post a Comment

 
Top