Mama mzazi wa aliyekuwa muigizaji maarufu nchini, Marehemu Steven Charles Kanumba, Flora Mtegoha, 'Mama Kanumba'.
BAADA ya jina la aliyekuwa msanii nguli wa filamu Tanzania, Marehemu Steven Kanumba, kuonekana kupotea taratibu, mama mzazi wa msanii huyo, Flora Mtegoha amefunguka kuwa hataacha kumuenzi mwanaye siku zote za maisha yake.
Akipiga stori na Amani, mama Kanumba alisema kuwa japokuwa watu wataendelea kumsahau mwanaye lakini yeye ataendelea kumuenzi labda afe.
“Hata kama watu wengine watamsahau Kanumba,watashindwa kuendelea kumuenzi lakini mimi nipo na nitaendelea kumuenzi labda nife,” alisema mama Kanumba.
Post a Comment