Mrembo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Flora Mvungi ‘H-Mama’
MREMBO kunako filamu Bongo, Flora Mvungi ‘H-Mama’ amewashangaa wanaomsema pembeni kuwa kawahi kuchepuka na kukanusha vikali kuwa hakuwahi kufanya hivyo tangu afunge ndoa na mumewe, Khamisi Ramadhani ’H-Baba.’
Akifunguka ya moyoni kwa paparazi wetu,Flora alisema tangu wakutane na H-Baba kipindi cha uchumba wao hajawahi kumsaliti hata siku moja zaidi ya kudumisha uaminifu mpaka leo.
“Nawashangaa wanaosema kuwa nimewahi kuchepuka jambo ambalo nalichukia sana maishani mwangu. Kwa sasa nafurahia sana maisha ya ndoa pia namshukuru Mungu tumebahatika kupata watoto wawili Tanzanite na Afrika.
Unajua wanawake wengi wanakosa utulivu na kushindwa kudumu na badala yake uachika muda mfupi kutokana na tamaa, ushauri wangu kwa wanawake wenzangu walio kwenye ndoa waheshimu nafasi hiyo wasifanye kama fasheni,” alisema Flora.
Post a Comment