Brighton Masalu
STAA ‘mtulivu’ wa uigizaji Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameibuka na kudai kuwa kama mwanamke aliyekamilika, anasikitishwa sana kwa kutopata mtoto hasa kutokana na kunyoshewa vidole na maneno mengi juu ya suala hilo.
Staa wa Bongo Movie , Ruth Suka ‘Mainda’ katika pozi.
Alisema kutokana na kukosa mtoto wakati mwingine hujisikia vibaya kiasi kwamba hutamani kuwabeba watoto wa wenzake, hasa wale wachanga wanaoanzia mwezi mmoja hadi mwaka huku akiamini kuwa wakati wake wa kuzaa umeshafika.
“Lakini wakati wa Bwana haujafika maana siwezi kuwa na mtoto bila ndoa, na wakati huo bado haujafika, unajua watu wananishangaza kwa kuninyooshea vidole kuwa sizai, natamani sana na Mungu atanipa kwa wakati wake,” alisema Mainda

Post a Comment

 
Top