Gladness Mallya
KABAANG! Zilipendwa wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amezua gumzo la aina yake baada ya kunaswa na ‘kidume’ kingine nchini Uganda.
KABAANG! Zilipendwa wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amezua gumzo la aina yake baada ya kunaswa na ‘kidume’ kingine nchini Uganda.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichowafuatilia wawili hao hatua kwa hatua, mpango mzima ulianzia jijini Mwanza ambapo Siwema alionekana akiwa na mwanaume huyo (jina halikupatikana mara moja) wakipeana kampani utadhani ni wapenzi.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, wawili hao walipanda basi la Friends jijini Mwanza ambapo Siwema na mwanaume huyo walikuwa beneti nje na ndani ya gari.
Kilieleza kuwa, wakiwa mpakani Mtukula wawili hao walikuwa wakipiga stori, kula chakula na vinywaji pamoja ambapo walipofika Kampala, Uganda walikatiza mitaani na kufikia kwenye Hoteli ya HBT.
“Nimesafiri na Siwema na mwanaume wake huyo kutoka Mwanza hadi Kampala yaani ni mahaba niue, kwani hata pochi alikuwa amebebewa na huyo mwanaume na kule walifikia hoteli ya HBT, nami nilikuwepo hapo kama siku nne hivi nikaondoka na kuwaacha, naona waliamua kwenda kupumzika huko,” kilisema chanzo hicho ambacho hata hivyo, kilishindwa kuthibitisha kama wawili hao walilala chumba kimoja.
Wakikatisha mitaa.
Baada ya kuzinyaka habari hizi paparazi wetu alimtafuta Nay wa Mitego ambaye ni mzazi mwenzake na kumweleza kuhusu hilo ambapo alisema mwanamke huyo siyo mkewe hivyo anao uhuru wa kuishi vile anavyojisikia.
“Nimesikia hizo habari, mimi sidhani kama kuna tatizo kwa sababu kitu muhimu kwangu ilikuwa ni mtoto ambaye tayari ninaye, kwake imebaki stori, mawazo yangu hivi sasa ni jinsi ya kumlea mwanangu na si vinginevyo,” alisema.
Alipotafutwa Siwema ili kusikia anazungumziaje picha hizo zilizonyetishwa na chanzo chetu, simu yake haikuwa hewani. Jitihada zinaendelea.
Siwema na Nay wa Mitego walikuwa ni wapenzi wa muda mrefu na walijaaliwa kupata mtoto mmoja ambapo miezi kadhaa iliyopita walimwagana baada ya Nay wa Mitego kumfumania mwanadada huyo na mwanaume mwingine
Post a Comment