Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha
BAADA ya vuta nikuvute ya wazazi wa wanafunzi, Hilary na Hamis ‘watoto wa Diamond’ walioshinda katika shindano la kucheza Ngololo mwaka jana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuahidi kuwasomesha katika shule ya East Africa International iliyopo Mikocheni, Dar huku akishindwa kuwalipia ada na watoto hao kurudishwa nyumbani, hatimaye wamerejeshwa tena shuleni.

Ilidaiwa kwamba wamewakataza kuzungumza kwenye vyombo vya habari kutokana na kwamba walichukizwa na habari hiyo kuvuja na kuripotiwa na gazeti hili kwa mara ya kwanza.
“Wale watoto wamerudi shule tayari baada ya kukaa nyumbani kwa miezi kadhaa, naamini hata gazeti lenu lilisaidia sana kuwashtua kwani vinginevyo wasingerudi na ndiyo maana hata wazazi waliambiwa wasiongee na ninyi,” kilisema chanzo hicho.
Naye mmoja wa wazazi wa watoto hao kwa sharti la kutokutajwa alisema: “Kwa sasa niko safarini ila ni kweli watoto wamerudi shule ila mambo bado hayajawa mazuri sana, sema ndiyo wako kwenye mazungumzo zaidi na suala hilo nimewakabidhi ndugu zangu ambao wako eneo la tukio ili walishughulikie.”
Post a Comment