Mrembo na mwanamitindo, Khloe Kardashian.
Las Vegas, Marekani
HAKUNA kulaza damu! Unaweza kusema hivyo kufuatia mrembo na mwanamitindo, Khloe Kardashian, kupata mpenzi mpya James Harden ambaye ni mcheza kikapu wa NBA kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa mumewe wa ndoa, Lamar Odom.
Khloe alionekana akiwa na staa huyo wa Ligi ya Kikapu ya Marekani anayechezea timu ya Houston Rockets, wakiwa ‘close’ huko Las Vegas wikiendi iliyopita, hali iliyotafsiriwa kuwa ni wapenzi.
Khloe na James walionekana wakiwa kama kumbikumbi Jumamosi iliyopita huko Red 8 katika mgahawa wakipata chakula cha usiku kabla ya kuondoka na kuelekea kwenye klabu moja ya usiku ambako msanii Chris Brown alikuwa akitumbuiza.
James Harden.
Harden alikuwa mmoja kati ya makocha wa tamasha la mpira wa kikapu kwenye sherehe ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Kanye West lililofanyika hivi karibuni.

Post a Comment

 
Top