Lagos, Nigeria
BOSI na prodyuza wa kampuni la  Mavin Records,  Don Jazzy, amesema anategemea mwanamuziki  Tiwa Savage, ajifungue mapema ili aweze kuendeleza harakati za kampuni lake katika ‘kutengeneza fedha’.
Don Baba J, kama prodyuza huyo anavyojulikana, na ambaye ni meneja wa Tiwa, aliandika kwenye mtandao wa Instagram kwa mwanamke huyo aliyevuma na wimbo wa ‘Eminado’ kwamba: “Mpenzi mtoto wa Tiwa Savage, njoo haraka duniani, mama yako anataka kuendelea na kazi.”
Tiwa ambaye sasa yuko London, Uingereza, akijitayarisha kujifungulia huko, alitangaza kupata ujauzito wake wa kwanza Januari 1, mwaka huu na akafanya sherehe ya kujitayarisha kumpokea mtoto anayetegemewa kuzaliwa Mei 17 mwaka huu jijini Lagos.

Post a Comment

 
Top