Meneja Huduma wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Dawit Mekonnen (wa pili kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni Ofisa Mauzo Mkuu wa shirika hilo, Lima Dsilva (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi (katikati) na Meneja Huduma wa Utalii, Philip Chitaunga.
 Viongozi hao wakisikiliza maswali kwa wanahabari (hawapo pichani).
Wanahabari wakichukua matukio.
ONESHO la kimataifa la utalii lijulikanalo kama Swahili International Tourism Expo’ (Site) linatarajiwa kufanyika kati ya Oktoba Mosi hadi 3, mwaka huu kwenye Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, meneja huduma wa utalii wa onesho hilo, Philip Chitaunga amesema kuwa tayari maandalizi ya kuelekea ufunguzi wa onesho hilo yanaendelea kuapamba moto.
Alisema kuwa wananchi wajiandae katika maonesho hayo ambayo yatakuwa ya kipekee tofauti na miaka iliyopita kwani kutakuwa na vivutio vingi ambavyo wananchi watajionea.
Alisema Mamalaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) na Shirika la Ndege la Ethiopia ndiyo wadhamini wa onesho hilo linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Post a Comment

 
Top