neyo3

Baada ya uvumi kuenea kuwa muimbaji wa R&B, Ne-Yo na mpenzi wake aitwaye Crystal Renay kuwa wamefunga ndoa na wanatarajia kupata mtoto, Ne-Yo ametoa ukweli.
Kupitia Twitter Ne-Yo amekiri kuwa ni kweli mchumba wake Crystal ni mjamzito na wanatarajia kupata mtoto, lakini amekanusha kuwa bado hawajafunga ndoa lakini amemchumbia na wanatarajia kufunga ndoa mwakani.
Aliandika:
“Clearing the air..@mscrystalrenay and I are ENGAGED to be married next year. And yes we are expecting. #FromTheHorsesMouth”
Kabla Ne-Yo hajathibitisha juu ya uvumi wa kufunga ndoa, Entertainment Tonight waliripoti kuwa chanzo kimoja kiliwathibitishia kuwa Ne-Yo na mchumba wake Crystal Renay wamefunga ndoa kwa siri, na kuongeza kuwa wanatarajia kupata mtoto


Post a Comment

 
Top