Spurs imefanikiwa kumsajili winga mshambuliaji aliyekuwa katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani Son Heung-Min ambaye ni raia wa Korea Kusini kwa mkataba wa miaka 5 baada ya kumfanyia vipimo vya afya na kufuzu. Dau la pound milioni 21.9 lilitosha kuishawishi klabu ya Bayer Leverkusen kumuachia winga huyo.
Tottenham Hotspur inamleta Son Heung-Min aliyeifungia Bayer Leverkusen magoli 21 katika mechi 58 za Bundesliga ili aje kushirikiana na Harry Kane ambaye ni mshambuliaji wa kati tegemeo kwa klabu ya Tottenham Hotspur.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za
Post a Comment