Klabu ya soka ya Simba imeendelea kujizatiti kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa kusajili wachezaji tofauti tofauti na sasa imemleta Justice Majabvi kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Vicem Hai Phong F.C ya Vietnam amewasili alfajiri ya August 1 katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Majabvi ametua Dar es Salaam kwa ajili ya kujiunga na Simba Sports na amepanda boti moja kwa moja kuelekea visiwani Zanzibar kujiunga na timu hiyo ambayo imeweka kambi visiwani humo kabla ya kurejea Dar es Salaam August 6.
Hata hivyo taarifa zinaripoti kuwa Majabvi atakuwa na muda wa siku tatu wa kufanya mazoezi na timu kabla ya kusaini mkataba ili kocha wa Simba Dylan Kerr amuangalie uwezo wake.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 amewahi kuichezea timu ya Dynamos na kufikia hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2008, kwa mara ya kwanza alicheza timu ya taifa ya Zimbabwe July 15 2004 dhidi ya timu ya taifa ya Zambia.
CHANZO CHA STORY HII>>>BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
Post a Comment