Mwanamuziki wa Nigeria, Waje.
MWIMBAJI wa kike wa Nigeria, Waje, amefuta ziara yake aliyokuwa aifanye Afrika Mashariki kutokana na kifo cha bibi yake kilichotokea majuzi. Ziara hiyo ilikuwa ifanyike tangu Julai 2 hadi Julai 6 mwaka huu.
“Mashabiki wangu wa Tanzania na Uganda nasikitika kuwajulisha kwamba ziara hiyo imefutwa. Nawaomba radhi kwa hali hiyo, hata hivyo mambo yatapangwa upya. Kifo cha bibi yangu kimenilazimisha kufuta ziara hiyo ya Afrika Mashariki.
“Ninasikitika kufuta ziara ya Tanzania na Uganda,  natumaini wapenzi wangu mtanivumilia ambapo nitakuja kuwa nanyi Tanzania na Uganda.  Nawatakia Baraka zote.  Asante sana,” mwimbaji huyo mrembo aliandika kwenye akaunti yake.

Post a Comment

 
Top