Mwenyekiti wa Taifa wa Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu Tanzania linaloundwa na wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM), Bi Zainabu Abdalah Issa akitoa tamko la umoja huo lililolenga kuwakumbusha wanachama wa chama hicho waliotangaza nia ya kuwania kuteuliwa kwenye nafasi ya Urais kuwa hakuna aliye maarufu au mwenye nguvu kuliko chama bali mgombea wa chama hicho atapatikana kwa mujibu wa taratibu na kanuni za chama na si vingenevyo.(Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO).
Mwenyekiti wa Taifa wa Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu Tanzania linaloundwa na wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) Bi Zainabu Abdalah Issa akiwa na wajumbe wa shirikisho hilo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo jijini Dar es salaam.
Frank Mvungi
Shirikisho la vyuo vya elimu ya juu Tanzania linaloundwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi limesema kuwa miongoni wa wanachama 42 walioomba kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hicho hakuna aliye maarufu au mwenye nguvu kuliko chama hicho.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bi. Zainabu Abdalah Issa wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
“Shirikisho la vyuo vya elimu ya juu tuna imani kubwa na wajumbe wote wa vikao vyote vya maamuzi ndani ya chama chetu kwa kuwa watatuteulia mgombea safi, muadilifu, na mzalendo atakayedumisha umoja na mshikamano ndani na nje ya chama chetu”alisisitiza Zainabu.
Akifafanua bi Zainabu amesema watia nia 42 wana Nafasi sawa katika uteuzi ambapo ni jambo la wazi kuwa wapo watakaokidhi vigezo na wapo watakaoshindwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu za uteuzi ndani ya chama cha mapinduzi (CCM).
Pia Zainabu alitoa wito watia nia wote 42 kuwa mgombea atakayepitishwa na vikao vyote vya maamuzi ndio atakuwa mgombea wetu wote na itakuwa ni jukumu la kila mwanachama kumsemea na kumnadi kwa Watanzania wenzetu ili CCM iendelee kuongoza Tanzania.
Akizungumzia mfumo wa kutoa maamuzi ndani ya chama cha mapinduzi Zainab amesema kuwa CCM ni Taasisi iliyoundwa kwa Muundo wa kuongoza kwa pamoja na kutoa maamuzi kwa pamoja dhana inyodhihirisha kuwa Chama cha mapinduzi si mali ya mtu binafsi au taasisi ya mtu mmoja inayotarajiwa kumfurahisha mtu huyo.
Shirikisho hilo linakipongeza chama hicho, kwa kuendelea kutekeleza demokrasia kwa vitendo kwa kuwapa wanachama wake kushiriki kwenye nafasi zote za uongozi ndani ya chama kwa ajii ya Uchaguzi Mkuu wa mwezi octoba 2015.
Post a Comment