Kocha mkuu wa Leicester, Nigel Pearson ametimuliwa kazi jana usiku baada ya kutofautiana na mmiliki wa klabu hiyo.
Wajumbe wa kikosi hicho wanaamini mahusiano hayo yamevunjika kutokana na mtoto wake Pearson,  James kuvunjiwa mkataba katika klabu hiyo kwasababu za kibaguzi wakati wakiwa kwenye ziara ya nia njema huko Mashariki ya Mbali.
Pearson aliiokoa Leicester kushuka daraja msimu uliopita na alitajwa kuwa kocha bora wa mwezi Aprili.
Timu yake ilikaa siku 140 mkiani mwa msimamo wa ligi, lakini ilishinda mechi saba kati ya tisa za mwisho na kumaliza nafasi ya 14 kati ya timu 20.

Post a Comment

 
Top