MWANAMUZIKI nyota wa Nigeria, Davido, amesema ukosefu wa mafuta nchini humo uliotokea miezi ya Mei na Juni mwaka huu ambao ulisababisha matatizo makubwa, ulimfanya alazimike kuahirisha kutoa albamu yake mpya hivi karibuni.
Akizungumza na televisheni ya Notjustok, Davido alisema pia kwamba huwa anachanganya lugha za nyimbo zake akiwa nje ya Nigeria, hususan Marekani, ambako hutegemea kupata mashabiki wengi na fursa zaidi za kupiga shoo nyingi.
Alisema pia mahafali yake ya kumaliza chuo ambayo ilifanyika mwezi Juni pia ulikuwa kipingamizi cha kutoa albamu yake hiyo mpya.
Post a Comment