Tangu maafisa kadhaa wa FIFA kutuhumiwa kwa rushwa siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo, kumekuwa na maneno maneno kuwa uwenda raisi huyo yumo kwenye ‘kapu’ hilo.
Lakini Blatter amekuja juu na kuwataka wanaomtuhumu kuthibitisha tuhuma zao kabla ya kumtuhumu na sio kuongea kitu wasichokuwa na ushahidi nacho.
“Watu hawajui neon wanalolitumia wanaponituhumu kwa rushwa. Mtu anayenituhumu lazima kwanza awe na uthibitisho juu ya hilo” alisema Blatter.
“Lakini hakuna wa kuthibitisha kuwa mimi ni mla rushwa kwa sababu sio (mla rushwa). Na atakayesema Blatter ni mla rushwa kwa sababu tu FIFA ina rushwa, ninachoweza kufanya ni kuwatikisia kichwa tu,” aliongeza Blatter.
Blatter ameendelea kusisitiza kuwa maneno yanayosemwa hataraji kama ya athari yoyote katika soka na anachukulia kama uchafuzi wa maisha yake binafsi.
“Tuhuma hizi juu yangu hazina uhusiano wowote na soka, ni shambulio kwa maisha yangu binafsi,” alisisitiza raisi huyo

Post a Comment

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top