Gari Aina ya Pro Box ikiwa tayari kusafirisha abiria |
Wakazi wa Mkoa wa Geita maeneo ya Buseresere na Katoro wapo katika hatari kubwa ya maisha yao kutokana na usafiri wanaoutumia kutoka eneo moja kwenda jingine.
Mwakilishi wa kikundi cha usalama barabarani Fungo Agustus ametutumia tukio hili ambalo ni hatari kwa abiria mkoani Geita.
Gari ndogo aina ya Pro Box zimeingia kwa wingi mkoani Geita na kutumika kubebea abiria katika mazingira ambayo si salama na ni hatarishi kwa abiria hao.
Abiria wamekuwa wakipakiwa kwenye mabuti ya kuwekea mizigo tena kwa msongamano mkubwa.
Zifutazo chini ni picha za kinachoendelea kwenye usafirishaji eneo la Buseresere.
Abiria wakiwa wamekusanywa kwenye buti eneo la kubebea mizigo huku wakiwa sambamba na watoto wadogo.
Aina nyingine ya Gari ndogo inayotumika kubebea abiria.
Mizigo na Watoto wakiwa wamekusanywa pamoja na mizigo nyuma ya Gari hiyo.
Post a Comment