Mkurugenzi2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Edwin Amandus Ngonyani kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico). Uteuzi huo umeanza Jumapili iliyopita, Juni 28, 2015.
Taarifa ya kuthibitisha uteuzi huo iliyotolewa Ikulu, Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) leo, Jumanne, Juni 30, 2015, inasema kuwa kabla ya uteuzi  wake Mhandisi Ngonyani alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Migodi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico.
Mhandisi Edwin Ngonyani ni mhandisi wa migodini mwenye uzoefu wa muda mrefu wa sekta ya madini. Anayo shahada ya kwanza ya fani hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Zambia na shahada ya uzamili (MSC) kwenye fani hiyo hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Exeter, Camborne School, Uingereza.
Mhandisi Ngonyani amefanya  kazi  nzuri wakati anakaimu nafasi ya Ukurugenzi Mtendaji na kwa kumteua, Rais Kikwete ana imani kubwa kuwa ataendeleza kazi hiyo nzuri ya kuimarisha uwekezaji wa umma katika sekta hiyo ya madini kupitia Stamico.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
30 Juni, 2015

Post a Comment

 
Top