Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Fomu zake za kuwania urais, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhwavi, wakati alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu wa CCM mjini Dodoma jana kwa ajili ya kurejesha Fomu za kuwania urais katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal. (Picha na OMR).
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipongezwa na Waziri wake wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Binith Mahenge, baada ya kurejesha Fomu za kuwania urais, katika Ofisi za Makao Makuu wa CCM mjini Dodoma jana juni 15, 2015 kwa. Katikati ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia wanachama wa CCM, wakati akitoka kwe ye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma jana, wakati alipotoka kurejesha Fomu za kuwania urais katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu. Nyuma yake ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal.
Post a Comment