Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, atakuwa mgeni rasmi katika Siku ya Wahandisi Tanzania itakayoanza Septemba 3 hadi 4, mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya siku hiyo, Profesa Bakari Mwinyiwiwa wsakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dares Salaam.
 Aliongeza kuwa kwa mwaka huu siku hiyo inaadhimishwa kwa mara ya 13, ambapo lengo lake ni kuwaonesha  umma kuwa wahandisi hao wanaweza kufanya katika kuleta maendeleo ya nchi, mchango wao wa maendeleo ya kijamii  na kiuchumi nchini.
 Malengo mengine ni kuwawezesha waajiri wa wahandisi na watumiaji wa huduma za kihandisi kutambua uwezo wa wahandisi   wazalendo na  kampuni za ushauri wa kihandisi za kizalendo, kuwatambua  wahandisi, kampuni na mashirika ya kihandisi yaliyotoa michango mikubwa ya kiuhandisi katika maendeleo ya taifa na hivyo kuwahamasisha wengine wengine kufanya shughuli zao vizuri.
Kuwahamasisha wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea uhandisi ili wafanye vizuri katika masomo yao na kuwafanya vijana washawishike kusomea masomo ya taaluma hiyo.
 Alizitaja miongoni mwa mada zitakazojadiliwa kuwa ni, majadilianoi ya kitaaluma, kiapo cha wahandisi wataalamu, maonyesho mbalimbali ya kiufundi na biashara na kuwatambua wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mitihani yao 2014/2015.
 Mada ndogo zitakazojadiliwa  ni maendeleo ya miundombinu, viwanda, ukuzaji na uwezo, kilimo na viwanda vya uzalishaji.

Post a Comment

 
Top