Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea jumla ya rufaa 54 za Wabunge kupinga Maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini. Pia jumla ya rufaa 200 za madiwani kutoka kwenye kata za Halmashauri mbalimbali.
Tume inaendelea kupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Wagombea (warufani) na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka Halmashauri mbalimbali. Pia imeanza kuzitolewa maamuzi rufaa za Wabunge tarehe 31/8/2015. Leo tarehe 01/9/2015 zimejadiliwa na kuamuliwa rufaa za Madiwani 53.
Kati ya Rufaa hizo Rufaa za kupinga kuenguliwa zilikuwa 9 na Tume imewarejesha wagombea Udiwani 8 na mmoja (1) Tume imetoa maamuzi kuwa kutenguliwa kwake ni sahihi. Aidha, Rufaa 44 zilikuwa za kupinga maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi na zote Tume imezitolea maamuzi ya kuridhika na maamuzi ya wasimamizi wa Uchaguzi. Hivyo, Rufaa 44 zimekataliwa na wagombea wataendelea na kampeni zao.
Tume inaendelea na vikao vya kusikiliza na kuamua Rufaa zilizosalia na itakuwa inatoa taarifa mara kwa mara.
Post a Comment