Daniel Korona akisherehesha hafla fupi ya kumuaga Balozi wa Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake Mhe. Amina Salum Ali iliyoandaliwa na Jumuiya ya Diaspora kutoka Afrika wanaoishi Montgomery county iliyofanyika siku ya Jumatano Sept 2, 2015 Silver Spring, Maryland.
Kulia ni mwongozaji maswali Bi. Soffie Ceesay ambaye ni mwanachama mwanzilishi wa Montgomery County’s African Affairs Advisory Group na African Immigrant Caucus akimuuliza Mhe. Amina Salum Ali maswali mbalimbali likiwemo nini anajivunia kwenye uongozi wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani. Balozi Amina Salum Ali alieleza ni ushirikiano wa nyanja mbalimbali mabazo nchi za Afrika zimenufaika na kupata mafanikio na uhusiano wa AU na Marekani kwa kuwezesha kupata Balozi wao nchini Marekani na kikubwa kabisa katika historia ya AU na yeye kama Balozi kuwezesha Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza katika historia kama Rais wa Marekani kuhutubia Umoja huo.
Isiah Leggett ambaye ni Montgomery County Executive akimtunukia cheti Mhe. Balozi Amina Salum AliBalozi Amina Salum Ali akitoa shukurani zake ambapo leo anaondoka kurudi Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani kazi aliyoifanya tangia 2006.
Wahudhuriaji
Wageni waalikwa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Post a Comment