Ben-Pol-2
Ikiwa ni siku ya pili toka sheria ya makosa ya mtandaoni ianze kutumika rasmi, Ben Pol amedai si rahisi watu kuacha tabia za kuchafua au kutukana wenzao mara moja.
Akizungumza na Bongo5 leo, Ben Pol amesema yeye tayari alishaacha na tabia ya kusoma kile kilichoandikwa na mashabiki wake kwenye mitandao kwa kuamini wengine wapo kwaajili ya kumkatisha tamaa.
“Watu hawawezi kuacha kuandika vibaya au vizuri,” amesema Ben Pol.
“Pia naamini yale matusi ya direct yatapungua kwa kiasi kikubwa. Mimi zamani hata kama sheria haijaanza niliachaga kuangalia vitu ambavyo vinaweza nikatisha tamaa, zinakuumiza yaani. Kwahiyo tuangalie matokeo ya sheria labda hali itabadilika,” aliongeza muimbaji huyo wa Sophia.

Post a Comment

 
Top