Kama uliwahi kukerwa na ishu ya wizi wa Baiskeli, basi wataalamu watatu wamekuja na majibu yote mtu wangu..!!
Cristóbal Cabello, Andrés Roi Eggers na Juan José Monsalve waliachana na masomo ya Chuo wanaweka nguvu yao wote kwa pamoja kwenye project ya kutafuta Ufumbuzi wa tatizo la wizi wa Baiskeli… wote watatu ni raia wa Chile.
Hasira yao ilitokana pia na mmoja wao kuibiwa baiskeli yake!! Wakaona isiwe tabu, project yao ilipata ufadhili wa kama dola laki moja hivi (sawa na Tshs. 210,000,000/=), nguvu yao ikazaa matunda ya kutokea hii baiskeli ambayo unaweza kucheki kwenye picha hapa pamoja na kipande cha video kinachoonesha unavyoweza kuifunga na ikabaki salama kabisa.
Post a Comment