WAKATI Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukielekea ukingoni, staa wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amekwea pipa kuelekea nchini China akidaiwa kumfuata bwana wake kwa ajili ya kwenda kufanya maandalizi ya Sikukuu ya Idd.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba mwanadada huyo kwa sasa amepata mpenzi ambaye makazi yake yapo nchini China ambapo amemuita kwa ajili ya kwenda kufanya maandalizi na kula Sikukuu ya Idd.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa Mwalumu Julius Kambarage Nyerere.
“Hivi hamjui kwamba Nisha sasa hivi mambo yake ya kifedha siyo mabaya kwani ana mpenzi mwenye hela sana anaishi China na ndiye amemwita huko japokuwa anawadanganya watu kwamba anaenda kufanya filamu, leo (Jumanne iliyopita) nasikia anasafiri muwahini Air Port,” kilisema chanzo hicho.
Post a Comment