Hali ya sintofahamu imeibuka katika eneo la Magomeni, Wilaya ya Bagamoyo baada ya mwili wa marehemu Hatujuani Shaaban kushindikana kuzikwa kutokana na ndugu zake kudai ulikuwa ukitokwa jasho, kutingisha miguu, kichwa na mikono wakati ukitayarishwa kwa maziko.
Kutokana na hali hiyo mwili huo ambao ulikuwa uzikwe jumapili uliachwa hadi jana baada ya daktari kuitwa na kuishauri familia, ndipo zoezi la mazishi likafanyika.
Hatujuani alifariki dunia katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo jumapili saa mbili asubuhi na mwili wake kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Ndugu yake aitwaye Mlau Mzee alisema walipofika nyumbani maandalizi ya mazishi yalianza kufanyika kwa taratibu za dini ya kiislamu na walitarajia kuuzika siku hiyo hiyo ya jumapili.
Alisema taratibu za kuosha mwili wa marehemu zilishindikana kutokana na maiti hiyo kujinyoosha, kutikisa kichwa na mguu wa kulia hali iliyowafanya wasitishe zoezi hilo na kumwita daktari.
Mzee alisema baada ya mwili huo kaachwaa juzi, hatimaye jana waliamua kumsafisha tena ambapo marehemu alitikisa tena mkono na ndugu kuamua kuwaita waganga wa kienyeji.
Daktari msadizi wa hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo Ally Ponza alikiri kutokea kwa kifo cha mtu huyo baada ya kumpokea akiwa na malaria kali na baadaye alifariki.
Alisema alipigiwa simu na muuguzi kuwa mama huyo amefariki na yeye kwenda kumpima na kuhakikisha amefariki kabla ya kuwaambia ndugu zake.
MTANZANIA
Post a Comment