Mayasa mariwata
GARI aina ya Toyota IST lenye thamani ya shilingi milioni 13 alilotaka kulitoa bure msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu `Bozi’ kwenda kwa msanii wa Bongo Fleva, Ally Salumu `Ally Nipishe’ limezua utata kila kona ya jiji. Amani linamwaga ubuyu.
Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu `Bozi’.
Tangu taarifa hizo zienee, wadau mbalimbali wa muziki na filamu wamekuwa njia panda huku wengine wakihoji kapata wapi hela kwa kipindi kifupi.
“Hakuwa hivyo, Bozi nimeanza kumfuatilia kipindi kirefu na huwa namuona mara kwa mara akitumia usafiri wetu wa daladala siku nyingine Bajaj, sasa ana jeuri gani mjini ya kumnunulia gari mwanaume?” alihoji Juma Mongolla mkazi wa Tabata.
Fatuma Ayubu `Bozi’ akilia baada ya Ally Nipishe kukataa zawadi ya gari.
Amani lilimtafuta Bozi ili kusikia kauli yake kuhusu gari hilo ambapo alifunguka;
“Mimi ni mtoto wa kike siwezi kufa njaa hapa mjini, maisha yangu kwa sasa ni mazuri kwani nina mwanaume mwenye pesa anayeniwezesha katika biashara zangu.
“Sifahamiani kabisa na Ally ila nikiwa kama shabiki wake katika muziki, niliguswa na matatizo yaliyompata ndiyo maana nikaona nimpe zawadi ya gari,” alisema Bozi.

Post a Comment

 
Top