Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na akiongea na wananchi wa Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam juu ya Mpango Shirikishi wa kuendeleza ardhi na makazi ya wananchi kwa kushirikiana na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angellah Kairuki akisisitiza namna mabaraza ya ardhi yanavyopaswa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa, wakati wa mkutano wa Waziri wa wizara hiyo na wananchi wa kata ya Makongo jijini Dar es salaam. Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Makongo Deusdedith Mtiro.
Diwani wa Kata ya Makongo Deusdedith Mtiro akimkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na ujumbe alioambatana nao wakati wa ziara ya kikazi iliyokuwa na lengo la kuongea na wananchi wa Kata ya Makongo kuhusu namna bora ya kuwashirikisha wananchi katika kuendeleza ardhi ndani ya kata hiyo kwa maendeleo endelevu na yenye manufaa kwa pande zote mbili yaani wananchi na Serikali.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na ujumbe wake kwa kuahidi na kusisitiza kuwa kufanikiwa kwa mradi wa Makongo kutahamasisha mpango wa ushirikishwaji wa wananchi katika kuendeleza ardhi na kuwa na makazi bora ambapo kufanikiwa kwake kutahamasisha mpango huo kutekelezwa maeneo mengine ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Mkazi wa Makongo juu Bi Ritha Mbotto akimuuliza swali Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo pichani) wakati mkutano na wanchi wa kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwandishi wa habari wa TBC Edward Kondela.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiteta jambo na Naibu Waziri wake Angellah Kairuki wakati wa mkutano na wananchi wa kata ya Makongo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Makongo wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na ujumbe wake wakati wa mkutano na wananchi wa kata ya Makongo jana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwasikiliza wananchi na kubadilishana mawazo mara baada ya mkutano katika kata ya Makongo jana jijini Dar es salaam.
Post a Comment