Ndani ya wiki moja baada ya Serikali ya Marekani kupitisha Sheria ya kuruhusu Ndoa za jinsia moja kwa raia wake kumekuwepo na maoni mbalimbali kutoka kwa watu kuhusiana na maamuzi hayo.
Mmoja wa watu walioguswa na maamuzi hayo ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabeambaye ameeleza hisia zake baada ya maamuzi hayo kupitishwa.
Katika mahojiano na radio ya Taifa ya Zimbwabwe, Mugabe alisema hawezi kupingana na maamuzi ya nchi hiyo kwani ni sheria ambayo imepitishwa na Serikali na kama ni hivyo ataamua kufunga safari kwenda mpaka Washington kuomba kufunga ndoa na RaisBarack Obama.
Ameongeza kuwa, Serikali ya Marekani imekuwa ikiongozwa na wajinga ambao ni wafuasi wa shetani wanaoitukana taifa la Marekani akisisitiza Marekani imechafuka na wanaiendesha nchi kwa dhana zao binafsi ambazo ni potofu
Post a Comment