Brighton Masalu
BLANDINA Chagula ‘Johari’ ambaye ni mwigizaji mkongwe Bongo, amejuta kuachana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Donald Mwakamele ‘McDonald’ kwa kusema kuwa angeendelea naye, angekuwa mwanamke mwenye heshima.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, staa huyo alisema vurugu za kimapenzi anazokutana nazo kila mara, zimekuwa zikimfanya arudishe mawazo nyuma ya kwamba, angeendelea na uhusiano na McDonald, angekuwa na maisha yasiyokuwa na mateso ya kihisia.
Hata hivyo,…

Hata hivyo, bila kumtaja, Johari alisema mpenzi aliyenaye kwa sasa anampa ‘stresi’ nyingi kwa kumchanganya na wanawake tofauti, jambo ambalo hakuwahi kukutana nalo katika maisha yake ya kimapenzi na McDonald.
Alisema kuwa, licha ya kuwa ni muda mrefu tangu kutengana kwao, bado wana uhusiano wa kawaida, ikiwemo kusalimiana na kubadilishana mawazo ya kimaisha na kwamba kama mwanamke anayehitaji faraja ya kweli, huingiwa na maumivu ya kuukosa uwepo wa mwanaume huyo na haiwezekani kurudiana kwani McDonald ana familia.
“Unajua stresi za mapenzi ninazokutana nazo zinanifanya nikumbuke mbali sana, uhusiano wangu na McDonald ulikuwa wa furaha sana, mpenzi wangu wa sasa ananiumiza kwa mengi, lakini kubwa ni kunichanganya na wanawake wengi,” alisema Johari.
Licha ya kukataa kumtaja mpenzi wake wa sasa, huko nyuma Johari aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mwigizaji Chuchu Hans.
Post a Comment